arrow_back
All Announcements
weekly
push_pin
Pinned
Matangazo ya Kanisa 01 - 07 June 2026
calendar_today
May 31, 2026
person
Super Admin
picture_as_pdf
Attachment Available
VFVak1uz4Q3HmCyDTYeOKJOJ56kzBstaCjAo80QR.pdf
VIONGOZI WA ZAMU
01 –07 JUNI 2026
MCHUNGAJI
REV. WITNESS SWAI 0629 534 530
MZEE WA KANISA:
MR. REMIGIUS NGAIZA
WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU
WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI
SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE
07/06/2026:
MR. RODERICK LUTEMBEKA
MRS.RHODA BUNDARA
MCH. GREYSON NYANTAMBA
MASHEMASI WA ZAMU:
MR. GREGORY MUSHI
MR. HOSEA NTUNUNGURU
MRS IDDA MHINA
MR. ISACK SAKARANI
MATANGAZO
Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea
vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo
hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu
pamoja na mashemasi.
Kutakuwa na Ibada ya shukrani ya nusu mwaka pamoja na Ushirika wa meza ya Bwana tarehe 28.06.2026.
Washirika wote tujiandae na ibada hiyo yenye baraka.
Mchungaji kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana
ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae
zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson
Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri
chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba.
MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI
1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango
wa ujenzi kwa awamu hii ya sita B kutoa au kupunguza
ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendele. Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako na kwa vizazi
vyako.
2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:
015 0020374000 CRDB BANK.
Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH
PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU
TANGAZO IDARA YA WATOTO
Tarehe 12.06.2026 : Mkesha wa kusifu na kuabudu, maombi na kuonyesha vipaji vya watoto na
maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Mzazi njoo
tuwaombee watoto wetu.
Tarehe 15– 21 Juni 2026 wiki ya Idara ya watoto
na wanafunzi, kutakuwa na makambi hapa kanisani kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni
Ibada ya Jumatano na Ijumaa (HBCF) zitaongozwa na Idara ya watoto.Njoo na familia yako
yote upokee kutoka kwa Bwana.
Tarehe 21.06.2026 ni kilele cha sikukuu ya watoto, sare ziko tayari (Tshirt) bei ni Tzs 10,000.
TANGAZO LA NDOA
Kwa mara ya pili tunatangaza harusi kati ya kaka
Jovin Jonathan Jovitha na dada Emiliana Bruno
Kipeto wote ni washirika wa TAG Kinondoni
.Harusi itafanyika siku ya Jumapili tarehe
14/06/2026 hapa kanisani TAG Kinondoni.
KUWEKA WAKFU WATOTO
Jumapili ya tarehe 07.06.2026 kutakuwa na ibada
ya kuweka wakfu watoto hivyo kwa mshirika
yoyote ambaye bado hajaleta mtoto wake, anakaribishwa.