arrow_back
All Announcements
weekly
Matangazo ya Kanisa 15 –21 JUNI 2026
calendar_today
June 14, 2026
person
Super Admin
picture_as_pdf
Attachment Available
YVzkLLAe4ORi09LmoC07MqrYizglywHiFZ5KRjry.pdf
MCHUNGAJI
REV. JOSEPH ENOS 0652 889 852
MZEE WA KANISA:
MR. MATHIAS MSANGI
WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU
WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI
SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE
21/06/2026:
DR. YOTHAM MACKENZIE
DR. DICKSON MKOKA
MR. JOSEPH MAMUYA
MASHEMASI WA ZAMU:
MR. LADISLAUS MELKIZEDECK
MRS. MAGRETH KATUMBA
MRS. MARY C. ZONGELA
MRS. MARIAM KASEKA
MATANGAZO
Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea
vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo
hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu
pamoja na mashemasi.
Kutakuwa na Ibada ya shukrani ya nusu mwaka pamoja na Ushirika wa meza ya Bwana tarehe 28.06.2026.
Washirika wote tujiandae na ibada hiyo yenye baraka.
Sambamba na hilo pia siku hiyo ya tarehe 28.06.2026
kutakuwa na chakula cha pamoja, hivyo Ibada itakuwa
moja na itaanza saa mbili asubuhi.. Kwaya zote zijiandae kuhudumu zikiwemo WWK, CMF na Watoto
Mchungaji kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana
ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae
zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson
Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri
chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba.
MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI
1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango
wa ujenzi kwa awamu hii ya sita B kutoa au kupunguza
ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendele. Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako na kwa vizazi
vyako.
2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba:
015 0020374000 CRDB BANK.
Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH
PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU
ZAMU ZA MAOMBI YA WATENDAJI
Watendaji wote wa Kundi BETHELEHEMU mtakuwa zamu ya mfungo na maombi siku ya Jumamosi ijayo ya tarehe 20.06.2026. Watendaji wote
waliopo maeneo ya Mr. Remigius Ngaiza, Mrs.
Rhoda Bundara, Mch. Greyson Nyantamba na Mch.
Dickson Mkoka.
TANGAZO IDARA YA WATOTO
Tarehe 12.06.2026 : Mkesha wa kusifu na kuabudu, maombi na kuonyesha vipaji vya watoto na
maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Mzazi njoo
tuwaombee watoto wetu chai na maandazi
vitakuwepo
Tarehe 15– 21 Juni 2026 wiki ya Idara ya watoto
na wanafunzi, kutakuwa na makambi hapa kanisani kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni
Ibada ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa (HBCF)
zitaongozwa na Idara ya watoto.Njoo na familia
yako yote upokee kutoka kwa Bwana.
Tarehe 20/6/2026 siku ya kuhitimu kambi watoto
wote watakuja kanisani kuanzia saa tatu asubuhi
hadi saa kumi na moja jioni, chakula cha mchana
kitakuwepo.
Tarehe 21.06.2026 ni kilele cha sikukuu ya watoto, sare ziko tayari (Tshirt) bei ni Tzs 10,000.