Matangazo ya Kanisa 15 –21 JUNI 2026
arrow_back All Announcements
weekly

Matangazo ya Kanisa 15 –21 JUNI 2026

calendar_today June 14, 2026 person Super Admin
picture_as_pdf

Attachment Available

YVzkLLAe4ORi09LmoC07MqrYizglywHiFZ5KRjry.pdf

download Download PDF
MCHUNGAJI REV. JOSEPH ENOS 0652 889 852 

MZEE WA KANISA: 
MR. MATHIAS MSANGI 

WAZEE NA MAKATIBU WAO WATAKAOKU WA ZAMU, KUABUDU IBADA ZOTE MBILI SIKU YA JUMAPILI IJAYO TAREHE 21/06/2026: 

DR. YOTHAM MACKENZIE 
DR. DICKSON MKOKA 
MR. JOSEPH MAMUYA 

MASHEMASI WA ZAMU: 
MR. LADISLAUS MELKIZEDECK 
MRS. MAGRETH KATUMBA 
MRS. MARY C. ZONGELA 
MRS. MARIAM KASEKA 

MATANGAZO 
Wazee wote wenye mitaa mnahimziwa kutembelea vituo vyenu vya HBCF ili kujua maendeleo ya vituo hivyo na kuviimarisha, wakisaidiana na makatibu pamoja na mashemasi. 

Kutakuwa na Ibada ya shukrani ya nusu mwaka pamoja na Ushirika wa meza ya Bwana tarehe 28.06.2026. 
Washirika wote tujiandae na ibada hiyo yenye baraka. 

Sambamba na hilo pia siku hiyo ya tarehe 28.06.2026 kutakuwa na chakula cha pamoja, hivyo Ibada itakuwa moja na itaanza saa mbili asubuhi.. Kwaya zote zijiandae kuhudumu zikiwemo WWK, CMF na Watoto 

Mchungaji kiongozi anakumbusha tena kuwa vijana ambao wako kwenye mahusiano ya uchumba wasikae zaidi ya miezi mitatu bila kuonana na Mch. Dickson Mkoka pia wajitambulishe kwenye kamati ya kushauri chumba na kuhudhuria kwenye vikao vya chumba. 


 MICHANGO YA FEDHA ZA UJENZI 

1.Kwa neema ya Mungu ujenzi wa kanisa letu unaendelea, hivyo unatiwa moyo wewe uliye ahidi mchango wa ujenzi kwa awamu hii ya sita B kutoa au kupunguza ahadi yako ili kazi ya ujenzi iendele. Kumjengea Mungu nyumba ya ibada ni baraka kwako na kwa vizazi vyako. 

2.Unaweza kutuma mchango wako kwenda namba: 015 0020374000 CRDB BANK. Jina: KINONDONI REVIVAL CHURCH PAA LA KANISA, MUUJIZA WANGU

ZAMU ZA MAOMBI YA WATENDAJI 

Watendaji wote wa Kundi BETHELEHEMU mtakuwa zamu ya mfungo na maombi siku ya Jumamosi ijayo ya tarehe 20.06.2026. Watendaji wote waliopo maeneo ya Mr. Remigius Ngaiza, Mrs. Rhoda Bundara, Mch. Greyson Nyantamba na Mch. Dickson Mkoka. 

TANGAZO IDARA YA WATOTO 

Tarehe 12.06.2026 : Mkesha wa kusifu na kuabudu, maombi na kuonyesha vipaji vya watoto na maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu. Mzazi njoo tuwaombee watoto wetu chai na maandazi vitakuwepo 

Tarehe 15– 21 Juni 2026 wiki ya Idara ya watoto na wanafunzi, kutakuwa na makambi hapa kanisani kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni 

Ibada ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa (HBCF) zitaongozwa na Idara ya watoto.Njoo na familia yako yote upokee kutoka kwa Bwana. 

Tarehe 20/6/2026 siku ya kuhitimu kambi watoto wote watakuja kanisani kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, chakula cha mchana kitakuwepo. 

Tarehe 21.06.2026 ni kilele cha sikukuu ya watoto, sare ziko tayari (Tshirt) bei ni Tzs 10,000.